UMEBEBA TEMBO, SIO MBWA: ACHA KUJILINGANISHA NA WATU
*Tembo na mbwa walishika mimba siku moja.*
*Miezi 3 baadaye, mbwa akazaa watoto 6.*
*Miezi michache ikapita, mbwa akazaa tena wengine 8.*
*Akazaa tena. Na tena.*
*Ndani ya mwaka mmoja akawa na kizazi kikubwa. Watoto wake wakaanza kuzaliana hapo hapo.*
*Siku moja mbwa akamsogelea tembo na kumuuliza kwa dharau:*
_"Ndugu, una uhakika una mimba kweli? Tulishika siku moja. Mimi nimeshazaa mara 4. Nina watoto zaidi ya 20. Wewe hujazaa hata mmoja. Kuna shida gani?"_
*Tembo akatabasamu. Akamjibu kwa utulivu:*
_"Ndugu yangu, sikiliza. Mimi tumboni sijaubeba mbwa. Nimeubeba tembo."_
_"Nitamzaa baada ya miaka 2. Lakini akizaliwa, akigusa ardhi, dunia nzima itatetemeka."_
_"Watoto wako wanapoishiwa na chakula, wanakula takataka."_
_"Mwanangu akitoka, akitaka kuvuka barabara, magari yatasimama. Watu watashangilia. Watapiga picha."_
_"Watoto wako 100 hawana thamani ya mtoto wangu 1."_
*FUNZO KWA MWANAUME ANAYEJILINGANISHA:*
*1. ACHA KUHESABU WATOTO WA MWENZAKO.*
Mbwa anazaa haraka. Watoto wake ni wengi, lakini ni wa kawaida. Tembo anazaa mmoja baada ya miaka 2, lakini anazaa MTAWALA.
*Rafiki yako amenunua boda boda. Wewe bado unasave ya gari. Usilie. Unabeba gari, sio boda.*
*2. KILA KITU KIKUBWA KINACUKUA MUDA.*
Nyumba ya udongo inajengwa siku 3. Ghorofa inajengwa miaka 3.
*Kama maisha yako yanachelewa kufunguka, maana yake unajenga kitu kikubwa. SAJAS anataka matokeo ya kesho. MWANAUME anasubiri matokeo ya miaka 5.*
*3. THAMANI HAIPO KWENYE WINGI. IPO KWENYE UPEKEE.*
Mbwa 100 hawafiki thamani ya tembo 1.
*Biashara zako 5 za TZS 100K hazifikii biashara 1 ya TZS 10M.*
*Acha kukimbiza vitu vidogo vidogo. Jikite kwenye kitu kimoja kikubwa.*
*HIVYO SAFARI YAKO, ACHA KUILINGANISHA NA YA MTU MWINGINE.*
*Hakikisha ulichokibeba wewe dunia ikikiona itajua ni tofauti.*
*Wewe si mbwa. Umebeba tembo.*
*Swali kwako:*
*Je, wewe unajua unabeba nini tumboni mwako? Au unazaa tu mbwa kwa sababu unaona wenzako wanazaa?*
*Comment chini. Tupe ushuhuda.*
*#UkweliMchungu #TemboNaMbwa #Subira #Mafanikio
Comments
Post a Comment