SPY NA BOSS WA MILLION 5: SOMO LA KIKATILI KUHUSU KUJIAMINI, KAZI NA THAMANI YAKO

 

*UTANGULIZI:*  

Boss alimpa Spy million 5 akamwambia "usije kuchakachua". Spy akajibu "huniamini?" Boss akajibu "siwezi kumuamini mtu nisie mtegemea kwenye maisha yangu". 


 


Spy akakasirika. Akaacha kazi.  


*Swali:* Nani mjinga hapa? Spy au Boss?  

*Jibu:* Wote wana somo lao. Lakini wewe msomaji, ukosefu wa kujua somo hili ndio utakayekufanya uishi maisha ya kuomba omba.  


*STORY KAMILI YA SPY NA BOSS WA MILLION 5:*  

Boss mmoja alimuajiri Spy kuwa mfanyakazi wake wa ndani. Siku moja Boss alitoka kazini na kurudi nyumbani kwake na kusimamisha gari yake kwa nje ya nyumba na kupiga honi akimuita Spy.  


Alipofika, Boss alimkabizi Spy funguo za chumba chake na kumuambia nenda chumbani fungua kabati na uchukue fedha kiasi cha million 5. Spy akajibu sawa.  


Ile kupiga hatua moja mbele, Boss alimuambia Spy "chukua million 5 tu na usije kuchakachua hizo pesa kwa kabati". Spy akajibu "kwaiyo unasema hivyo huniamini Au?"  


Boss alimuambia Spy "siwezi kumuamini mtu nisie mtegemea kwenye maisha yangu". Spy akachukia kwa kusikia ya kuwa yeye sio chochote kwa yule Boss na akaondoka na kuacha ile kazi.  


*SOMO KUBWA LA UKWELI MCHUNGU:*  

*UMEJIFUNZA NINI HAPA? MIMI NIMEJIFUNZA KUWA SIKU ZOTE TUACHE KUJIAMINISHA KWA WATU WASIO TUTEGEMEA KWENYE MAISHA YAO.*  


Ngoja nikuvunje vipande 3:  


*1. KOSA LA SPY: ALITAKA HESHIMA ASIYO STAHILI*  

Spy alikuwa mfanyakazi wa ndani. Hakuwa mtoto wa Boss. Hakuwa mshirika wa biashara. Hakuwa ndugu. *Alikuwa mtu wa kulipwa mshahara.*  


Boss alikuwa na haki ya kutilia shaka. Million 5 sio Tsh 5,000. *Kuamini ni gharama.* Na Boss alichagua asilipe gharama hiyo kwa mtu asiye na uzito kwenye maisha yake.  


*Spy alikasirika kwa sababu alijiona "anastahili" kuaminiwa.* Hii ndio shida ya vijana wengi. Unataka heshima ya bosi wakati bado wewe ni "mfanyakazi". Jenga uzito kwanza.  


*2. UKATILI WA BOSS: ALISEMA UKWELI MCHUNGU*  

Boss hakumtukana Spy. Alisema ukweli: _"Siwezi kumuamini mtu nisie mtegemea kwenye maisha yangu."_  


Tafsiri yake: *"Wewe ni wa kunilipa, sio wa kunitegemea. Kwa hiyo sitaweka hatima yangu mikononi mwako."*  


Ni ukatili? Ndio. Ni ukweli? Ndio. *Dunia haijajengwa kwa hisia zako. Imejengwa kwa maslahi.*  


*3. SOMO KWAKO MWANAUME: ACHA KUOMBA KUAMINIWA. JENGA KUTEGEMEWA*  

Acha kuomba watu wakuamini. *Jenga maisha yako mpaka watu wakutegemee.*  


1. *Kazini:* Usilalamike bosi hakuamini. Fanya kazi yako mpaka ofisi ishindwe kufanya kazi bila wewe. Siku hiyo watakulinda kama dhahabu.  

2. *Kwenye Mahusiano:* Usimuulize mwanamke "mbona huniamini". Muonyeshe thamani yako mpaka akuogope kukuacha.  

3. *Kwenye Maisha:* Usijidai kuwa wa maana. Kuwa wa maana. Mtu wa maana haombwi kuaminiwa. Anategemewa.  


*HITIMISHO:*  

Spy aliondoka na hasira. Boss akaendelea na maisha yake. *Nani aliumia? Spy.*  


Kwa sababu Spy alichagua hasira badala ya somo. Angekaa, angejifunza, angejenga thamani, miaka 2 mbele angekuwa meneja. Badala yake, akarudi mtaani kusema "mabosi hawana utu".  


*Swali kwako leo:* Je, wewe ni Spy unayetaka kuaminiwa bila thamani? Au unajenga maisha yako mpaka watu wakutegemee?  


*TOA MAONI YAKO HAPO CHINI:*  

1. Boss alikosea kumwambia Spy hivyo au alikuwa sahihi?  

2. Ungekuwa wewe ni Spy, ungefanya nini? Ungeondoka au ungekaa?


Kama somo hili limekuchoma, acha comment "NIMEJIFUNZA". Share kwa mwanaume mwenzenu aliye kazini. 


Unataka masomo kama haya kila siku yanayojenga ubongo na mfuko?  tufollow Instagram @Lazenji 


Comments

Popular posts from this blog

CHUKUA ELFU 50,000: SIRI YA KUTOFANIKISHA MAISHA YAKO

ULIISHA ACHWA KISA HUNA PESA? HII NDIO SABABU MWANAUME TAJIRI HAACHIKI.