FRIENDZONE NI UJINGA: NILIKUBALI KUWA RAFIKI YAKE KWA MIAKA 3, NILICHOJIFUNZA KILINIUA

 

Wanaume wengi wamekufa kiroho kwa sababu ya neno moja: "TUENDELEE KUWA MARAFIKI". 



Leo nakusimulia kisa cha Spy, kijana aliyejenga urafiki kwa miaka 3 na binti aitwaye Judith. Mwisho wake? Alipoteza rafiki, akapoteza mpenzi. Na alijifunza somo linaloua wanaume wengi kimya kimya.


Kama una rafiki wa kike unayempenda kwa siri, kaa chini. Hii ni kwa ajili yako.


*Jinsi Spy Alivyoingia Mtegoni Bila Kujua*


Kukutana na mtu mara kwa mara hujenga urafiki. Spy alikutana na mdada mmoja anajulikana kwa jina la Judith. Spy alikutana na Judith kwa kila siku kwenye mishe mishe zake, hivyo wakatengeneza urafiki kwa kila mmoja kumwamini mwenzake.


Spy alikuwa bega la Judith la kulilia. Alimsaidia assignment usiku wa manane, alimkumbusha kunywa dawa, alijua anapenda chips mayai na pilipili nyingi. Kwa miaka mitatu, Spy alijenga imani. Alidhani anajenga msingi wa mapenzi. Kumbe alikuwa anajenga gereza lake mwenyewe. Kila "asante kaka" kutoka kwa Judith ilikuwa msumari mwingine kwenye jeneza la matumaini yake.


*Siku Alipouwa Urafiki kwa Mkono Wake*


Baada ya miaka mitatu, Spy alivutiwa na matendo ya Judith. Moyo haukuvumilia tena. Siku hiyo Spy akajiambia kuwa natamani siku moja Judith awe mpenzi wangu. Mwaka ulio fuata Spy akashindwa kuvumilia na akaona bora amwambie Judith ya kuwa anampenda.


Judith baada ya kusikia yale maneno kutoka kwa rafiki yake anayemheshimu na kumwamini, alichukia sana na kumtusi Spy. Alimwambia, "Sikutegemea hili kutoka kwako. Nilidhani wewe ni tofauti. Umeharibu kila kitu." 


Spy alijisikia aibu na kuamua aondoke na kuishi mbali na Judith. Hivyo akajikuta anapoteza vyote yaani kapoteza rafiki yake kipenzi na mtu ambae anampenda.


*Gharama ya Miaka 3 ya "Urafiki Mtakatifu"*


Spy hakupoteza Judith. Alijipoteza mwenyewe. Miaka mitatu ya muda, pesa, na hisia zilikufa ndani ya dakika tano za ukweli. Aibu ilimfanya ajifungie ndani kwa miezi. Hakuweza kumtazama usoni mtu yeyote aliyemjua na Judith.


Huo ndio mshahara wa uoga. Unakaa kimya kwa jina la "kuheshimu urafiki" wakati moyo wako unapiga kelele za mapenzi. Mwisho wake unapoteza vyote viwili. Duniani hakuna hasara kama ya mwanaume anayekufa na hisia zake.


*Sheria 3 za Spy za Kuepuka Friendzone Milele*


Umejifunza nini hapa? Mimi nimejifunza kuwa siku zote hakuna urafiki kati ya mwanamke na mwanamume kama mmoja ana hisia. Hizi ndio sheria za kujikinga:


1. *Sheria ya Siku 7:* Ukiwa na hisia kwa mtu, sema ndani ya siku 7. Urafiki mrefu sio heshima. Ni kuchelewa. Mwanaume wa kweli anapiga nia mapema. Akikataa, umeokoa miaka 3 ya maisha yako.

2. *Sheria ya Kuuza Thamani, Sio Urafiki:* Usinunue mapenzi kwa kuwa "available" 24/7. Usimpelekee lunch kila siku ukitegemea siku moja akupende. Huo ni mradi wa hasara. Kama anakupenda, atakutafuta hata ukiwa busy.

3. *Sheria ya Kataa Majina ya Gereza:* Mtu akikuanza kukuita "kaka", "bestie", au "mdogo wangu" wakati wewe una hisia, mkate mara moja. Mwambie, "Sipendi hilo jina." Hayo ni majina ya kukufunga usiweze kutoka. Mwanaume anaitwa kwa jina lake.


Wewe unaamini urafiki wa dhati kati ya mwanaume na mwanamke unawezekana? Au Spy yuko sahihi kuwa ni uongo? Tuambie uzoefu wako wa friendzone hapo chini. Comment itakayogusa watu wengi nitampa zawadi ya Tsh 5,000.

friendzone, urafiki mwanaume na mwanamke, mapenzi, kuvunja urafiki, somo la spy na judith, mahusiano, ukweli mchungu, kuacha friendzone

Comments